Press Releases

UONGOZI Institute’s Women’s Leadership Forum will convene in Dar es Salaam for the fifth time today, under the theme “The contribution of women to leadership in Africa”. The guest of honour will be Dr. John Jingu, Permanent Secretary for the Ministry of Community Development, Gender, Women, and Special Groups (Tanzania). Dr. Linda Ncube-Nkomo, Chief Executive Officer of the Nelson Mandela Children’s Fund (South Africa), will deliver the keynote address.
Kongamano la Wanawake katika Uongozi la Taasisi UONGOZI litafanyika leo kwa mara ya tano Jijini Dar es Salaam, chini ya dhima ya “Mchango wa wanawake katika uongozi barani Afrika”. Mgeni Rasmi wa Tukio hili atakuwa Dkt. John Jingu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum (Tanzania). Wasilisho kuu litatolewa na Dkt. Linda Ncube-Nkomo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Watoto ya Nelson Mandela (Afrika Kusini).
Dar es Salaam: The first-ever forum for UONGOZI Institute’s alumni will be held today at the Dar es Salaam Serena Hotel. Eng. Zena Ahmed Said, Chief Secretary and Secretary of Revolutionary Council of the Revolutionary Government of Zanzibar, will officiate the event. The keynote address will be delivered by Mr. Omari Issa, Chancellor of the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology.
Dar es Salaam: Kongamano la kwanza la wahitimu wa Taasisi UONGOZI litafanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena. Mgeni Rasmi wa Tukio hili atakuwa Eng. Zena Ahmed Said, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Wasilisho kuu litatolewa na Bw. Omari Issa, Mkuu wa Chuo cha Afrika cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Dar es Salaam: UONGOZI Institute will hold its eighth graduation ceremony at the Mlimani City Conference Centre in Dar es Salaam, today. The guest of honour will be Hon. George Boniface Simbachawene (MP), Minister of State, President’s Office – Public Service Management and Good Governance. The keynote address will be delivered by Mrs. Suzanne Innes-Stubb, First Lady of Finland and a renowned international expert in the fields of law and ethics.
Dar es Salaam: Sherehe ya mahafali ya nane ya Taasisi UONGOZI itafanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi wa Tukio hili atakuwa Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Wasilisho kuu litatolewa na Bibi Suzanne Innes-Stubb, Mke wa Rais wa Finland na mtaalamu mwandamizi wa kimataifa katika masuala ya sheria na maadili.
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ALF Patron and fourth President of the United Republic of Tanzania, and H.E. Hailemariam Dessalegn Boshe, former Prime Minister of the Federal Democratic Republic of Ethiopia, will convene the 8th African Leadership Forum (ALF) at the Speke Resort Munyonyo, Kampala from 7 – 8 April 2025.
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mlezi wa Kongamano la Kikanda la Viongozi wa Afrika na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mhe. Hailemariam Dessalegn Boshe, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, wataitisha Kongamano la 8 la Kikanda la Viongozi wa Afrika Jijini Kampala kuanzia tarehe 7 – 8 Aprili 2025.